clock

,,,,,

Saturday, September 29, 2012

Elewa maana Halisi Ya Neno IQ

Definition: Intelligence is defined as the ability to adjust to one's environment. It also can be defined as the power to make correct responses from the standpoint of truth and fact. Thus, we may say that intelligence is an indicator of the ability to cope successfully with novel situations. Measurements: The level of intelligence an individual has is measured by the difficulty of the task he can perform. the range or worth of action he can do so the speed with which he can do so Meaning of I.Q: It is a ratio between Mental Age and Chronological Age multiplied by 100. I.Q= (Mental Age/Chronological Age) * 100 Example: A five year old child with a mental age of six will have an I.Q of 120 I.Q=6/5 * 100 = 120 I.Q indicates the rate of mental growth of a child. It expresses the size of yearly increments that are made to a child's mental level. So, it may be regarded as an index of intelligence. However, children with the same I.Q may differ in M.A and C.A. IQ Classification Above 140 Genius or near genius 120-140 Very superior intelligence 110-120 Superior intelligence 90-110 Normal intelligence 80-90 Dullness 70-80 Borderline below 70 Definite learning disability

Jiridhishe na Elimu ya Anga kwa ufupi

Masuala ya angani ni ya ajabu na ya kumvutia kila mtu kiasi cha kuamini kila kitakachowekwa mbele yetu kwa kutumia taswira za Mwezi mkubwa, mkusanyiko wa nyota zinazomeremeta, na magimba ya angani yenye maumbo ya ajabu na ya kutatanisha, na kadhalika. Matukio mawili ya hivi karibuni yanaonesha umaasuma wetu katika kuamini habari yoyote inayotolewa, ikichanganyika na shauku tunayopata kwa kusikia habari za maajabu ya angani. Lakini je hayo maajabu kweli yanaweza kutokea? Je tumejiuliza ukweli wa maelezo tuliyosikia? Mkanganyiko wa kwanza ulitokea mwezi uliopita tarehe 31 Agosti, ulikuwa unahusu kuwapo Miezi miwili ya rangi ya bluu. Baadhi ya tovuti katika mtandao, zilionesha Mwezi mpevu uliowekewa rangi ya bluu. Kwa bahati nzuri, usiku wa tarehe 31 Agosti, hakukuwa na Mwezi wa rangi ya bluu ila ulionekana Mwezi mpevu mmoja unaong’ara kwa mwanga mweupe kama unavyo kuwa kawaida. Kilichotokea ni kwamba, kwa vile mzunguko mmoja wa Mwezi huchukuwa siku 29 na nusu, na mwezi mmoja kawaida una siku 30 au 31, inawezekana kwamba katika mwezi mmoja kukawa na Miezi pevu miwili. Hali hii hutokea kwa nadra sana, kwa wastani wa mara moja kila mwaka mmoja na nusu au mara moja katika siku 600 hivi, ambayo ni nadra sana. Katika semi ya Kiingereza, Mwezi mpevu wa pili katika mwezi kama huo huitwa “blue Moon” (yaani Mwezi bluu) kutokana na usemi wao “Once in a blue Moon” (yaani, “mara moja katika Mwezi bluu”). Usemi huu hutumika kuelezea tukio ambalo si la kawaida. Haina maana kwamba rangi ya Mwezi itabadilika - ni usemi tu wa Kimombo. Kisayansi haiwezekani kabisa kwa Mwezi kugeuka kuwa rangi bluu. Mwezi mpevu wa kwanza katika Agosti ulikuwa tarehe 2 na Mwezi mpevu wa pili ulitokea tarehe 31 Agosti. Kwa hiyo usiku wa tarehe 31 Agosti, baadhi ya watu ambao hawaelewi kuwa rangi ya Mwezi haiwezi kubadilika kuwa bluu walikiri kwa msisitizo kuwa waliona Mwezi mpevu ukiwa na rangi bluu!! Kwa vile Agosti ilikuwa na Miezi pevu miwili, wengine walidai kwa nguvu kuwa kulikuwa na Miezi pevu bluu miwili usiku wa tarehe 31 Agosti. Akili ikikubali utaona hata yasiyokuwepo. Tahadhari, na usiamini yote unayoona katika mtandao. Uzushi mwingine ambao unazungushwa kwa miaka zaidi ya minne inahusu Miale ya Cosmo itakayoingia Dunia LEO USIKU saa 6:30 usiku hadi saa 9:30. Miale inasemwa inatoka sayari ya Mirih (Mars) na kulipua simu yako kama imewashwa, na kukutahadhari uzime simu. Tatizo la usushi kama huu ni kuwa inahusu kitu cha kukudhuru LEO HII ambayo inaweza kuwa siku yoyote inaposemwa. Kwa hiyo kama usuzhi huu hauondoki, hata baada ya kuvuma kwa miaka minne sasa. Sayari ya Mirihi haina uwezo wa kutoa miale yoyote kwa vile Inang’aa kwa kuakisi mwanga wa Jua. Miale ya Cosmo (Cosmic Rays) hutolewa na Jua wakati wote, mara nyingine kwa ukali. Hata hivyo, Dunia yetu inalindwa dhidi ya miale hiyo kwa uga wa usumaku uliotuzungukwe (magnetic field envelope). Kwa hiyo ukisikia uzushi wa miale ya cosmo, ujue kuwa hauna ukweli wowote. Tuje sasa katika kisa kingine cha kusisimua kilichowapumbaza wasikilizaji, ingawa ni cha kuvutia. Tunaelezwa kwamba kutakuwa na kiza kwa siku tatu tarehe 21, 22 na 23 Desemba mwaka huu kwa vile siku hizo, ulimwengu wote utajipanga katika mstari na kusababisha Dunia kusimama katika mzingo wake nakusitisha mzunguko wake wa kuizunguka Jua. Ukweli ni kuwa ingawa siku hizo Dunia na Jua vitakuwa katika mstari mmoja na kitovu kikali cha Galaxy yetu, hali hii ya vitu vitatu hivyo kuwa katika mstari hutokea KILA Desemba, na siyo tu Desemba ya mwaka huu. Je, unajua kuwa Dunia inamwendo haraka kiasi gani? Inasafiri kwa kasi ya kilometa 100,000 kwa saa katika mzingo wake wa kuizunguka Jua. Pamoja na hiyo inazunguka katika mhimili wake kwa kiasi cha kilometa zaidi ya 1,000 kwa saa katika Ikweta. Sisi hatuhisi mwendo mkubwa kama huu kwa vile Dunia yetu ni kubwa mmno na tumegandwa Duniani na mvuto wa gravity. Sasa, jaribu kutafakari ugumu wa kusimamisha gari linalokimbia kwa mwendo wa kilometa 100 tu kwa saa, na utaelewa ugumu wa kusimamisha Dunia inayotembea kwa kasi ya zaidi ya kilometa 100,000 kwa saa. Hata kama Dunia ingeweza kusimama siku hizo tatu, bado itaweka nusu ya Dunia inayoangalia Jua kuwa katika mwanga wa mchana na nusu ya upande wa pili utakuwa katika kiza la usiku. Je Jua litaondolewaje siku hizo ikiwa Dunia nzima itatakiwa kuwa katika kiza? Ni jambo lisilowezekana kisayansi. Hata mtu mwenye elimu ya msingi ataweza kuona hicho ni kichekesho. Kwa nini watu wanakubali kisa kisichoaminika kiasi hicho? Hii ni kwa vile watu huvutiwa sana na mambo ya anga za juu na akili zetu ni ombwe zikisubiri kujazwa na visa vya aina zote. Habari nyingine iliyochangia suala hili ni tafasiri ya kuisha mwishoni mwaka 2012 kwa kalenda ya Wamaya (watu wa zama za kale walioishi Marekani ya Kusini). Ilisemwa kuwa kuisha kwa kalenda inamaanisha mwisho wa Dunia. Kutokana sababu kama hizi, wananchi wamekuwa tayari zaidi kudanganywa na visa mbali mbali yanayohusu anga za juu. Kukabili hali ya kukubili uzushi wa mambo ya anga za juu bila kudadisi vizuri, na ili tuweze kukata kiu yetu ya mambo ya anga, tuanzishe elimu ya anga na astronomia kuanzia ngazi za msingi na kuisuka katika mfumo wetu wote wa elimu, hadi elimu ya juu. Mwezi bluu mwingine unatarajiwa Julai 2015, ambapo Mwezi mpevu wa kwanza utakuwa Julai 2, 2015 na Mwezi mpevu wa pili (yaani Mwezi bluu) utakuwa tarehe 31 Julai, 2015. Muda bado upo. Tujitayarishe TUSIONE Miezi MIWILI yenye rangi ya BLUU Julai 2015.

Friday, September 28, 2012

Kumbe Inawezekana Mume Kupata dalili za mimba ya Mke

Ni kawaida kwa wanawake wengi wakati wa ujazito kuanza kutapika , kuwa ni kichefu chefu ,kuhisi kisunzi au kizunguzungu , kujisikia mnyonge, hasa wakati wa asubuhi. Wazungu wanasema ni Morning sickness. Wataalam wanasema haina sababu moja. Lakini wanakubali kuwa husababishwa na ongezeko la homoni hasa ya Estrogen katika mwili wa mwanamke ambayo inaweza kumuongezea , uwezo wa kusikia harufu hasa mbaya. Kuongezeka kwa maji aina ya gastroline. Na unafahamu kuwa mwanamume.Baba mwenye nyumba pia anaweza kuwa na dalili hizo hizo za ujauzito yaani ?, kizunguzungu,kutapika , kichef chefu , tumbo kufura na kuwa na hasira kama mkewe? Kwa wakati huu Mike Dowdall , bwana mwenye umri wa miaka 25 kutoka Manchester Uingereza amefura tumbo, anatapika tapika , asubuhi, husikia kisunzi au kizunguzungu na anapenda kula vitu vichachu kama maembe mabichi yalitiwa chumvi au pilipili. Kwa wakati huu mpenzi wake Amanda Bennett ni mjamzito. Dahili za Mike zilipoanza bi Amanada alichukulia kwamba mpenzi wake ambaye wameishia naye miaka mitatu anamfanyia mzaha au stihizai Eti anamuiga vile anavyo tapika, na kupenda kula kula. Lakini madaktari kutoka Manchester wanasema Bwana Mike ana ugonjwa wa mimba bandia. Wao wanaita Couvade syndrome huu sio uchawi , bali ni ugonjwa unaoweza kuwapata wanaume. Tumbo kufura, kutapika tapika asubuhi, kuhisi kizunguzungu na kupenda kula maembe ya liotiwa chumvi au pilipili. Mike amekuwa na uja uzito bandia kwa wiki 33 na kama vile tu akina mama walio na mimba , Mike ameongeza uzani au zaidi ya kila 3 na sasa anajihisi mchovu kila mara, kuumwa na mgongo na kwenda haja ndogo kila mara. Madaktari hao wanasema ugonjwa huu unaweza kusababishwa na ile hali kuwa wasiwasi unaposubiri mkeo kujifungua, au pia kuwa karibu sana na mkeo. Bi Amanda ambaye ana mimba ya wiki zaidi ya 34 sasa analazimika kumsugua mumewe mgongoni na kiunoni kila siku na kumkanda tumbo lake. Habari hizo zimeshamiri katika gazeti la The Sun la uingereza.

Wazijua kondom za zamani

Nani asiyejua kazi ya Kondom? Lakini unajua kifaa hicho ambacho siku hizo husambazwa bure kilianza lini na wapi? Tarehe yenyewe haifahamiki lakini katika karne ya 15 yaani miaka mia 6 iliyopita kondom zilikuwepo na zilikuwqa zinatumika katika bara la Asia. Miaka mia sita iliyopita Kondom nchini china zilikuwa nizatengenezwa kutumia utumbo au mbuzi au kondoo. Matajiri walikuwa wakitumia Kondom zilizotengenezwa kwa karatasi ya hariri iliyopakwa mafuta. Nako nchini Japan Kondom zilikuwa zikitengenezwa kwa magamba ya kobe au pembe za wanyama . Naama pembe ilikuwa ikivaliwa kama kondom..ni huko Japan, miaka mia 6 iliyopita. Ni katiuka karne iliyopita , mwaka 1900 kondom zilizotengenezwa kwa utumbo wa mbuzi na kondoo hata utumbo wa ngombe zilianza kuenea duniani. Enzi hizo ilikuwa inatumiwa kukinga magonjwa ya zinaa na kuzuia mimbia isiyotakikana.

Thursday, September 27, 2012

Hatimaye Sudan Zakubaliana

Sudan na Sudan Kusini zimetia saini makubaliano kuhusu biashara, mafuta na usalama ingawa hazijakubaliana kuhusu mipaka. Baada ya mazungumzo ya siku ya nne, nchi hizo mbili zimeafikiana kuruhusu usafirishaji wa mafuta kutoka kusini kupitia mabomba ya Kaskazini na kuondoa wanajeshi mpakani. Taarifa zinazohusiana Sudan Viongozi wa nchi hizo mbili hatimaye wamekubaliana baada ya mazungumzo ya siku nne mjini Addis Ababa Ethiopia. Lakin maswala kadhaa muhimu yangali kutatuliwa ikiwemo kuafikia makubaliano kuhusu mipaka inayozozaniwa ikiwa ni mojawapo ya kilichosababisha mgogoro ambao nusura utumbukize nchi hizo kwenye vita mapema mwaka huu.
Baada ya mapigano kuzuka kuhusu mzozo wa mafuta na mipaka, Umoja wa mataifa ulitishia kuziwekea pande zote mbili vikwazo ikiwa hazitaafikia makubaliano ya kina. Wapatanishi wa Muungano wa Afrika wangali kuthibitisha kuwa makubaliano yameafikiwa lakini rais wa Sudan Omar al-Bashir na mwenzake wa Kusini Salva Kiir, wanatarajiwa kutia saini makubaliano hayo hii leo. Maelezo yametolewa tu kwa mukhtasari lakini wapatanishi wa pande zote mbili, walisema kuwa wamekubaliana kuhusu eneo la nchi hizo mbili ambalo halina ulinzi wa kijeshi. Pia makubaliano ya kiuchumi yaliafikiwa kuruhusu Sudan Kusini kuanza tena shughuli zake za kuzalisha mafuta. Lakini mwafaka haukupatikana kuhusu eneo linalozozaniwa la Abyei wala mipaka mingine mingi ambayo nchi hizo zinazozania. Kwa hivyo makubalino hayo hayajaweza kutimiza masharti ya Umoja wa Mataifa kwa nchi hizo kuafikia mkataba unaotatua mzozo huo kwa kina.(At bbc swahili)

Uruguay Yahalalisha Utoaji Mimba

Bunge la Congress nchini Uruguay limepitisha sheria ya kuhalalisha utoaji mimba katika hali zinazokubalika. Bunge hilo limepitisha sheria hiyo kufuatia majadiliano makali yaliyoishia kwa wabunge hao wa Congress kuipitisha kwa kura 50 dhidi ya 49. Sasa hoja hiyo itawasilishwa katika bunge la juu la Senate ambalo linatazamiwa kuiidhinisha. Sheria hiyo itawaruhusu wanawake kutoa mimba kabla haijafika wiki 12 ilimradi wamepata ushauri nasaha kutoka kwa madaktari wasiopungua 3 ili kufahamishwa hatari za kutoa mimba. Mbali na Cuba, Uruguay itakuwa nchi ya kwanza katika ukanda wa Amerika kusini kuruhusu mwanamke yeyote anayetaka kutoa mimba fursa ya kufanya hivyo.

Tuesday, September 25, 2012

ULAYA YASITISHA MISAADA KWA RWANDA

Muungano wa Ulaya umeamua kusitisha msaada kwa Rwanda. Uamuzi wa Muungano huo umefikiwa kufuatia ripoti ya baraza la usalama la Umoja huo iliyodai kwamba Rwanda inaunga mkono waasi wa M23 dhidi ya serikali ya Congo. Waasi hao wanadhibiti kimabavu sehemu kubwa ya Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na hata kuwatoza kodi wananchi.
Kundi hilo lilianza uasi katika eneo hilo mwezi Aprili na kusababisha takriban watu nusu milioni kukimbilia usalama wao. Lakini Rwanda imeendelea kukana madai hayo. Umoja wa Mataifa unafanya mkutano na baadhi ya yatakayopewa kipaombele kwenye mkutano huo ni swala la mgogoro huo Mashariki mwa Congo. Mapema mwezi Julai Marekani ilizuia dola 200,000 zilizokusudiwa kulisaidia jeshi la Rwanda. Msaada wenyewe uliokatwa siyo mkubwa kwa jeshi la Rwanda, lakini hatua hiyo ilitoa ishara kubwa. Kwa kukata msaada huo, Marekani ni kama ilikuwa inasema "tunaamini ripoti kuwa Rwanda inatibua usalama wa kanda hiyo kwa kuwaunga mkono wapiganaji wa Congo". Mwezi Juni ,Umoja wa Mataifa ulikabidhi ripoti kwa Baraza la Usalama, ambayo ilisema ina ushahidi mzito kuwa Rwanda inalipatia kundi la M23, wapiganaji na zana, na kurahisisha makamanda wao wakubwa kusafiri na kuvuka mpaka baina ya Congo na Rwanda.
Wanawake Mashariki mwa Congo wakilaani maasi Uasi huo ulianza mwezi wa Aprili, wakati wanajeshi mia kadha wa jeshi la Congo walipofanya ghasia. Uasi huo uliongozwa na Jenerali Bosco Ntaganda, ambaye anasakwa na Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC, kwa uhalifu wa kivita. Nayo serikali ya Uholanzi ilisitisha msaada wa dola milioni 6.15 kwa Rwanda baada ya nchi hiyo kuhusishwa na madai hayo ingawa baadaye ilianza tena kutoa msaada kwa nchi hiyo baada ya serikali ya Rwanda kuahidi kushirikiana na kukomesha vita hivyo. (at BBC SWAHILI)

Mtu mrefu duniani ahitaji Mke

Pichani juu ni Sultan Kosen ambaye ndio mtu (mwanaume) mrefu kupita wote duniani kwasasa ambaye ameingia kwenye kumbukumbu za guinness toka February 2011. Sultan ana urefu wa 251 cm (8 ft 3 inch) na uzito wa 168.2kg na amezaliwa 10 December 1982 huko Mardin Turkey (Uturuki).Hapo yupo na aliyekua mtu mfupi kupita wote He Pingping ambaye kwasasa ameshakufa na amekufa akiwa na umri wa miaka 21, urefu wake ulikua 2 ft 5.37 in (74.61 cm) Sultan alipo ulizwa ni nini matumaini yake baada ya kuingia kwenye rekodi ya watu warefu akajibu ''napenda kusafiri kote duniani, kupata gari ambayo inanitosha na kuwa na watoto'' Sultan anasema anatafuta mchumba hivi sasa kwahio wadada mnaotaka kuolewa jaribuni bahati yenu!!

Aliyeongeza makalio aamua kuwapa somo wengine madhara yake

MWANAMKE aliyetumia zaidi ya dola 15,000 za Marekani (Sh22.5 milioni) kwa ajili ya kuongeza ukubwa wa makalio yake, sasa ameandika kitabu kuhusu kile alichokiita siri ya wanawake weusi kuchomwa sindano zenye sumu ili kuongeza ukubwa wa makalio yao. Vanity Wonder (30), raia wa Marekani ambaye ni mama wa watoto wawili, ameweka bayana kuhusiana na soko la vipodozi feki lililosheheni nchini humo na kuzidi kuingia katika Bara la Afrika ambalo limesababisha yeye kuathirika kutokana na sindano za kemikali ya Siliconi alizochomwa. "Ndani ya Kitabu changu cha ‘Shot Girls’, nimeelezea kuhusu ufahamu na uzoefu wangu katika shughuli hii ya kuongeza ukubwa wa makalio na jinsi gani nilivyochomwa sindano hizo na jinsi nilivyoweza kuwa msaidizi wa soko la vipodozi hivyo," alisema. Vanity anaelezea zaidi kuhusiana na mama aliyempeleka binti yake wa miaka 17 na kuweza kumchoma sindano ya kuongeza makalio pamoja na kutengeneza meno feki. "Manesi na wauguzi, polisi na waimbaji wa nyimbo za injili ni mojawapo kati ya wateja wetu wakubwa na walio wengi ni watu wale ambao wanajua fika kwamba kitendo hiki ni hatarishi," anasema. Vanity anaweka bayana sababu kubwa ya kumfanya aandike kitabu hicho ni kwa kuwa alitaka kuelezea hadithi yake yeye mwenyewe na kuwafafanulia wengi kuhusu imani potofu juu ya siri hii. Anasema mwaka 2006 ndipo alipoanza kuitafuta sehemu wanakochoma sindano za kukuza makalio na kufanikiwa kuipata, alipewa matibabu aliyoyataka lakini baadaye walimtaka awe mmoja wa watumishi wao. Anasema alikubali na kuanza kufanya nao. “Tulikuwa tunanunua kemikali ya ‘silicon’ katika vituo vya gesi," anasema. Anasema watu wengi huwaeleza wenzao uongo juu ya hilo, hivyo yeye aliamua kuwaacha watu wajaribu na kujionea wenyewe. “Ni kama kitu cha siri, najitahidi kuwaeleza watu kwa sasa kuliko kuwaacha wajaribu kama nilivyowaacha hapo awali.” Alisema wanawake kuamua kujibadilisha maumbile yao ni kinyume cha sheria, tamaduni za makabila yote. Aliongeza kuwa kufanya hivyo pia kunawaweka wanawake katika hatari ya kupata maambukizi ya bakteria au hata kusababisha kifo. "Si kitu watu wanachofikiri,wapo baadhi ya wasichana ambao wanafanya hivyo kwa kuwa wamemwona mwenzao anafanya," anasema. Hivi sasa Vanity ambaye ni mama wa watoto wawili anasema si kwamba yeye ameridhika kuwa hivyo, bali ni kati ya wachache ambao hawajapata madhara makubwa kwa sasa na kwamba baada ya miaka kadhaa, anategemea atapata madhara makubwa hivyo anawaonya wale ambao hawajatumia wasiingie katika genge hilo. Mmoja wa madaktari wanaomtibu, Dk John Martin anasema sindano hizo hutumika kuongeza makalio, mashavu, hips na kwamba ni ghali sana. "Wakati mwingine hutumia madawa ya viwandani ambayo pia yanaweza kuwa sumu ikiwa mtumiaji atatumia kwa kiasi kikubwa na hivyo unaweza kuishia katika maisha ya taabu na wapo wengine ambao walikatwa sehemu ya viungo vyao na wengine kufa," anasema Dr Martin.(mwananchi.co.tz)

MZOZO CHINA NA JAPAN

Uchina na Japan zinafanya mazungumzo ya hali ya juu kuhusiana na visiwa vinavyozozaniwa katika ziwa la China Mashariki. Mkutano huu ni wa kwanza tangu kuanza kwa mzozo huu nchini China mapema mwezi huu. Taarifa zinazohusiana Siasa Kulingana na taarifa kwenye mtandao wa wizara ya mambo ya nje wa China, naibu waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Zhang Zhijun, amemuonya mwenzake wa Japan kuwa China haitaruhusu ukiukwaji wowote wa uhuru wa eneo lake. Mkutano huo unaoendelea mjini Beijing, unakuja wakati takriban mitumbwi sitini kutoka Taiwan ikisindikizwa na manowari za kijeshi kuingia katika visiwa hivyo vinavyozozaniwa upande wa China. Msafara huo wenye wavuvi karibu mia tatu uko katika maeneo ambayo Japan inamesema yanafaa kuwa na ulinzi. Mitumbwi hiyo iko na wanamaji wa Taiwan. Kisiwa hicho chenye utata --kinachoitwa Senkaku nchini Japan na Dia oyutai nchini Uchina -- kinadaiwa na Uchina, Japan na Taiwan. Uhusiano kati ya Uchina na Japan umeharibika katika wiki za hivi karibuni baada ya serikali ya Japan kununua visiwa vitatu kutoka kwa mmiliki binafsi. Uhasama wa hivi karibuni umetokea wakati wanadiplomasia wakuu kutoka nchi zote mbili wanakutana mjini Beijing kujadili mzozo wa mpaka. (bbc swahili)

IRAN YAIBANIA GOOGLE

Serikali ya Iran imebana huduma za mtandao wa tafuta tafuta wa Google,pamoja na huduma zake za barua pepe za Gmail. Afisaa mmoja wa serikali amesema kuwa hatua hiyo ilichukuliwa kama tahadhari kufuatia maandamano makubwa ambayo yalikumba nchi za kiisilamu zilizokerwa na filamu ya Marekani iliyomkejeli Mtume Mohammad na dini ya kiisilamu. Taarifa zinazohusiana Asia Filamu hiyo ilipeperushwa kupitia mtando wa kijamii wa YouTube ambao unamilikiwa na Google. Baadhi ya wanablogu, wamekemea hatua hiyo ya serikali kama inayolenga kukandamiza uhuru wa kujieleza Maafisa wa utawala wamekuwa wakijiandaa kuzindua mtandao mwingine wa internet utakaotumika tu nchini humo ilinwananchi wakome kutumia mitandao ya kigeni. Kwa mujibu wa maafisa wakuu, hatua hiyo italinda mtandao wa internet wa Iran kutokana na uvamizi kutoka nje.

Monday, September 24, 2012

Lijue Ziwa Tanganyika

Ziwa la Tanganyika ni kati ya maziwa makubwa ya Afrika ya kati ikiwa eneo lake ni la pili tu baada ya Viktoria Nyanza katika Afrika na ujazo wa maji yake ya pili duniani baadaya Ziwa Baikal. Jina lake limekuwa tangu 1919 pia jina la koloni ya Kiingereza ya Tanganyika. Ziwa lina ujazo wake mkubwa umetokana na vilindi vyake vinaelekea chini hadi mita 1470. Urefu wa ziwa ni 673 km na upana wake takriban 50 km. Maji ya Ziwa Tanganyika yanajaza ufa kubwa kwenye ganda la dunia ambalo ni sehemu ya bonde la ufa la Afrika ya Mashariki. Eneo la maji ni 32,900 km². Ziwa la Tanganyika limepakana na nchi zifuatazo: Kongo, Tanzania, Burundi na Zambia. Kongo na Tanzania zinatawala sehemu kubwa ya ziwa. Beseni ya ziwa ni 231,000 km². Mito miwili mikubwa ya Ruzizi na Malagarasi inapeleka maji yao ziwani. Maji yanatoka kwa njia ya mto Lukuga kwenda mto Kongo. Miji mikubwa ziwani ni mabandari ya Kigoma kwa upande wa Tanzania na Kalemie kwa upande wa Kongo. Kila bandari ni pamoja na mwanzo wa njia ya reli. Mji mkubwa kabisa ni Bujumbura mji mkuu wa Burundi.

Sunday, September 23, 2012

Walimu Kenya Waongezwa Mshahara

Kwa mara ya kwanza serikali ya Kenya imekubali kutoa nyongeza ya asili mia 300 kwa mishahara ya walimu ambao wamekuwa katika mgomo wa kitaifa kwa wiki tatu sasa. Taarifa zinazohusiana Kenya, Siasa Kutokana na maafikiano hayo kati ya serikali na chama cha walimu nchini KNUT, sasa walimu wanatarajiwa kurejea kazini Jumatatu. Hatua hiyo sasa itawapa afueni maelfu ya wanafunzi hususan wa shule za msingi na upili za umma ambao hawajafunzwa wakati huu walimu walipokuwa mgomoni. Vyama vya walimu nchini Kenya KNUT na Kuppet vilikuwa vikishinikiza serikali kuwalipa walimu nyongeza hiyo kwa awamu moja. Awali serikali ya Kenya ilikuwa imekataa kutekeleza matakwa hayo na kuwataka walimu kukubali kulipwa kwa awamu tatu, awamu ya kwanza ikitekelezwa Oktoba mwaka huu. Mwalimu wa chini aliyekuwa akipata shilingi 13,000 sasa atapata shilingi 39.000. Serikali ya Kenya imetenga zaidi ya dola 159 milioni kuwalipa zaidi ya walimu 250,000 ambao walikuwa wakigoma kulalamikia mishahara duni na mazingira mabaya ya kazi.

Friday, September 21, 2012

Makabiliano mpakani mwa Isrel na Misri

Mwanajeshi wa Israel na wapiganaji watatu wameuwawa kwenye mapigano mpakani baina ya Israil na Misri. Israel inasema wapiganaji walikuwa na silaha tele, na walifyatua risasi dhidi ya wanajeshi waliokuwa wakilinda wajenzi wanaorefusha uzio kwenye mpaka wa Israel. Inaarifiwa kuwa mpiganaji mmoja alirusha bomu.Kuna taarifa kuwa wanajeshi wengine kadhaa wa Israil walijeruhiwa. Hivi karibuni, jeshi la Misri lilifanya operesheni kubwa dhidi ya wapiganaji wa kiislamu upande wa mpaka wa Misri, baada ya shambulio Kaskazini mwa eneo la Sinai, ambapo wanajeshi 16 wa Misri waliuwawa.

Serikali ya KENYA na WALIMU

Serikali ya Kenya imetishia kuwafuta kazi walimu ambao wamekuwa wakigoma kwa wiki tatu sasa na kuwaajiri walimu wapya waliofuzu pamoja na walimu waliostaafu ikiwa hawatarejea kazini hii leo. Makataa hii inakuja baada ya vyama vya walimu kukataa pendekezo la nyongeza ya mishahara ambayo wangelipwa kwa awamu tatu. Taarifa zinazohusiana Kenya Walimu hao wanataka nyongeza ya aslimia miatatu ya mishahara, pesa ambazo serikali inasema haiwezi kumudu kwa sasa kwa sababu ya hali mbaya ya kiuchumi. Mgomo wa walimu umesababisha kufungwa kwa shule za umma kwa zaidi ya wiki tatu sasa wakati wanafunzi wakijiandaa kwa mitihani ya kitaifa. Huenda serikali ikalazimika kuakhirisha mitihani hiyo ya kidato cha nne na darasa la nane inayotarajiwa kuanza katika muda wa wiki chache zijazo. Madaktari wa hospitali za umma pia wanafanya mgomo wa kitaifa huku hospitali hizo zikiwahudumia tu wagonjwa walio katika hali ya dharura.

Wednesday, September 19, 2012

Mlipuko Kiwandani Mexico Waua 26

Takriban watu 26 wameuawa Kaskazini mwa Mexico baada ya mlipuko na kisha moto kuzuka katika kiwanda cha gesi katika jimbo la Tamaulipas. Kampuni ya mafuta ya serikali ya Mexico,Pemex imeeleza kwamba moto huo ulitokea katika kiwanda hicho nje ya Reynosa iliyo karibu na mpaka na Marekani. Taarifa zinazohusiana ajali Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, Juan Jose Suarez, alisema kuwa watu ishrini na tano wlaiuawa katika kiwanda hichho huku mmoja akikanyagwa na gari. Wafanyikazi wengine wengi walijeruhiwa. Akizungumza katika mkutano na waandishi habari, Juan Jose Suarez Coppell alisema kuwa tayari wameanzisha uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha mlipuko huo Visa kama hivyo, vimewahi kutokea katika viwanda vilivyoko karibu vya Pemex katika miezi miwili iliyopita ambavyo vimesemekana kutokea kutokana na wizi wa mafuta unaotekelezwa na makundi ya wahalifu.

Rais Obama Na Rafikiye Mtoto wa Uganda

Kijana Christopher Kule, mwenye umri wa miaka kumi na ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi wilayani Kasese, nchini Uganda, hajaachwa nyuma katika ndoto hiyo. Taarifa zinazohusiana Afrika Bila shaka wengi watasema yuko hatua nyingi mbele ya wale walio na ndoto ya kumuona Obama. Hii ni baada ya Kule kupokea majibu ya barua aliyomwandikia Rais Barack Obama kutoka kwa Obama mwenyewe. Kijana huyo anaamini kuwa baada ya kuandikiana barua na Rais Obama, kuna matumaini kwamba siku moja atakutana naye. Yote haya yanatokana na zoezi la kuandika barua ambalo Kule na wanafunzi wenzake walikuwa wanafanya darasani, baada ya kuagizwa na mwalimu wamwandikie barua mtu yeyote wakiomba msaada kwa jamii yao. Barua ya Kule bila shaka ilimtia hamasa mwalimu wake wa kigeni kutoka Marekani ambaye alikuwa anafunza shuleni humo kwa muda. Mwalimu huyo alisema kuwa nyanyake ni rafiki wa mmoja wa wasaidizi katika ikulu ya rais na kuahidi kuhakikisha kuwa ujumbe huo utamfikia rais Obama na bila shaka ahadi ikatimizwa , kwani barua ilimfikia rais Obama. Kule alisema kuwa katika barua yake, alimwomba Obama kusaidia Uganda kuangamiza uasi na kuhamasisha amani. Katika majibu yake kwa Kule, rais Obama alisema kuwa Marekani imejitolea kuangazia maswala kadhaa muhimu kote duniani kama haki za binadamu kwa sababu Marekani inapinga vikali ghasia na ukandamizaji dhidi ya watu wote. Pia alimtumia kijana huyo picha yake aliyokuwa ametia saini. Rais Obama alipata muda wa kumjibu kijana Kule. Je marais wa Afrika wana muda wa kuzungumza na wananchi wao na kutoa mfano wa Obama kwa Afrika?

Friday, September 14, 2012

SOMA HII KAMA WAKOSA USINGIZI

Tatizo la kukosa usingizi huenda likawa ishara ya kutambua mapema maradhi ya kusahau au ''Alzheimer'' kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa kutumia panya ambaye ana maumbile yanayofananishwa na binadamu. Vipande vya protini, kwa lugha ya kitaalamu (plaques) au uchafu kwenye ubongo yanadhaniwa kuwa sehemu nyeti inayosababisha maradhi haya. Taarifa zinazohusiana afya Utafiti uliofanywa na kuchapishwa katika jarida la tafsiri ya matukio ya Sayansi, umeonyesha kuwa punde chembe chembe za uchafu ule ulipoanza kukua kwenye ubongo wa panya, usingizi ukaanza kuwa tatizo kwa viumbe hao. Taasisi inayosimamia utafiti wa maradhi hayo, (Alzheimer's Research UK) imehimiza kuwa ikiwa uhusiano huo unaweza kuthibitishwa huenda ikawa muhimu kwa Madaktari. Utafiti wa kutaka kugundua mapema kama mtu anaelekea kukumbwa na maradhi ya Alzheimer inadhaniwa kuwa muhimu katika kutibu maradhi hayo. Wagonjwa hawaonyeshi dalili kupitia hisia au kumbukumbu zao hadi baada ya mda mrefu wa maradhi kumkumba mgonjwa. Yanapofikia hapa sehemu za ubongo huwa zimeharibika kiasi kwamba tiba inakua vigumu kupatikana au hata kushindwa kupatikana. Ndiyo sababu wataalamu wanafanya juhudi za kuanza mapema kugundua kama mtu atapata maradhi haya, miaka kadhaa kabla ya dalili hizo kujitokeza. Viwango vya protini ijulikanayo kama Beta Amyloid kimaumbile hupanda na kushuka miongoni mwa binadamu na pia panya katika kipindi cha saa 24. Hata hivyo ni ile protini ambayo hujenga uchafu usiofutika kwenye ubongo na maradhi ya Alzheimer. Majaribio yaliyofanywa katika Chuo Kikuu cha Washington yameonyesha kuwa panya wanaotoka usiku kwa kawaida hulala kwa dakika 40 kwa kila saa mchana. Lakini ubongo ulipoanza kupatwa na uchafu panya hawa wakaanza kusinzia kwa dakika 30 pekee. Ugonjwa wa sahau Mmojapo wa wataalamu, Prof David Holtzman, alisema: "endapo mapungufu katika usingizi huanza mapema kiasi hiki katika ugonjwa wa Alzheimer, mabadiliko hayo yanaweza kutupa ishara ya wepesi wa kuweza kuyatambua maradhi haya." "ikiwa matatizo haya ya usingizi yapo, hatuelewi hasa yanachukua mfumo gani, kupungua kwa usingizi kikamilifu au ni tatizo la kushindwa kabisa kulala au ni kitu tofauti kabisa." Hata hivyo, utafiti unaofanyika kwa kutumia panya mara nyingi hayafai kutumika kwa binadamu kwa sababu nyingi zinazosababisha kutatizika na usingizi. Dr Marie Janson, kutoka shirika la kujitolea Alzheimer's Research UK, ametaka utafiti zaidi ufanywe kwa kuwapima binadamu kuona kama kuna uhusiano baina ya matatizo ya kukosa usingizi na ugonjwa wa Alzheimer. Aliongezea kuwa: "tayari umekuwepo utafiti unaounganisha mabadiliko katika usingizi huchangia katika matumizi ya ubongo kwa fikra, lakini matokeo haya yanaonyesha kuwa kuna uwezekano wa kuwa mapungufu katika usingizi pia inaweza kuwa ishara na onyo la maradhi ya kusahau au Alzheimer.

EBOLA YAITESA DRC

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mlipuko wa homa ya Ebola, katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imefika watu 31 hadi kufikia sasa na hata inatishia kuathiri miji kadhaa. Taarifa zinazohusiana Afrika Hili ndilo onyo limetolewa na shirika la afya duniani WHO. Mipuko wa kwanza wa homa hiyo uliripotiwa tarehe kumi na saba mwezi wa saba katika mkoa wa Kaskazini Mashariki wa Orientale. Afisaa mmoja wa shirika hilo Eugene Kabambi aliambia shirika la habari la Reuters kuwa hali ni mbaya sana na kwamba bado haijadhibitiwa. Ni rahisi sana kuambukizana homa ya Ebola na homa hiyo huuwa asilimia tisini ya watu ambao huambukizwa. Hakuna tiba inayojulikana kwa homa hiyo wala chanjo. Homa hiyo husambaa kwa kugusana na husababisha mgonjwa kuvuja sana damu. Idadi ya vifo vilivyotokana na homa yenyewe katika miji ya Isoro na Viadana, imeongezeka maradufu kwa zaidi ya wiki moja hadi watu 31. Homa ya Ebola Inaarifiwa wauguzi watano wamefariki kutokana na homa hiyo. "homa hii bado haijadhibitiwa. Badala yake hali ni mbaya zaidi hata kuliko awali. Ni mbaya sana'' alisema bwana Kabambi. "ikiwa hakuna hatua zitachukuliwa sasa hivi, homa hiyo itasambaa hadi maeneo mengine na hata katika miji mikuu,'' aliongeza Bwana Kabamba. Mwezi jana mlipuko wa aina mbaya sana ya homa hiyo katika nchi jirani ya Uganda ilisababisha vifo vya watu 16 lakini wafanyakazi wa afya wanasema kuwa milipuko hiyo miwili haina uhusiano wowote.

wakati huo huo

Waandamanaji walioghadhabishwa na filamu inayodhihaki dini ya kiisilamu wameshambulia balozi za Uingereza na Ujerumani mjini Khartoum, Sudan. Waandamanaji walianza kuwasha moto na kisha kuichanachana bendera ya Ujerumani na kuweka bango lenye maandiko ya kiisilamu ambapo bendera hiyo ilikuwa. Taarifa zinazohusiana Afrika Maandamanao yangali yanaendelea katika nchi za Mashariki ya kati na Kaskazini mwa Afrika kuilaani filamu ya Marekani inayokejeli Mtume Muhammad. Mjini Cairo, polisi waliwarushia gesi ya kutoa machozi na kuwatawanya waandamanaji takriban 500,kutoka katika ubalozi wa Marekani. Maandamano pia yalifanyika katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa. Msemaji wa ubalozi wa Uingereza amethibitisha BBC kuwa maandamano yanafanyika nje ya ubalozi wa Uingereza na kusema kuwa polisi wa Sudan wako katika eneo hilo kudhibiti hali. Hata hivyo, msemaji huyo hangeweza kuthibitisha ikiwa waandamanaji waliingia katika ubalozi huo au ikiwa maandanamo yana uhusiano wowote na filamu hiyo inayopingwa na waisilamu kote duniani.

KUZAGAA KWA MAANDAMANO MPAKA SUDAN

Afisa mmoja wa ubalozi wa Marekani ameuawa na wengine wamejeruhiwa wakati kundi la watu waliojihami na silaha walipovamia jengo hilo mjini Benghazi. Inaaminika kuwa watu hao walikuwa wanaandamana kulaani filamu mmoja iliotengenezwa nchini Marekani ambayo wanasema inamkejeli Mtume Mohammed. Taarifa zinazohusiana Libya Jengo hilo liliteketezwa kabisa na wandamanaji hao waliokuwa na hasira. Maandamano hayo yalichochea makabiliano kati ya vikosi vya serikali na kundi la wanamgambo maarufu kama Ansar al Sharia brigade, mjini Benghazi. Msemaji wa serikali ya Marekani, amelaani kitendo hicho na ameongeza kuwa wanashirikiana na idara ya usalama nchini Libya kuimarisha usalama kwenye balozi zake. Taarifa zinasema kuwa wakaazi wa mji mkuu Tripoli, wamekuwa wakishawishiwa kupitia ujumbe kwenye tovuti za kijamii wafanye maandamano lakini hakuna aliyejitokeza. Sehemu ya filamu hiyo inasambazwa kupitia mtandao wa Youtube kwa lugha ya kiarabu. Maandamano sawa na hayo pia yamefanyika mjini Cairo nchini Misri. Kundi lingine la watu limeingia kwenye ubalozi wa Marekani na kuteketeza bendera ya nchi hiyo. Taarifa kutoka Cairo zinasema, maelfu ya Waislamu na Wakristo wameungana kulaani filamu hiyo. Hata hivyo hakuna aliyejeruhiwa kwenye maandamano hayo yaliofanyika Misri.

Wednesday, September 12, 2012

Shambulio kwa rais mpya wa SOMALIA

Kuna shambulio la mauaji katika mageti ya hotel somalia ya Mogadishu.Shambulio hilo la bomu lilikuwa limekusudiwa kwa raisi mpya wa nchi hiyo ya Somalia bwana Hassan Sheikh Mohamud ambapo ndipo alipo.
Shambulio hilo ambalo inasemekana limeua watu saba wakiwemo watu wawili waliohusika na shambulio hilo.Pia miongoni mwa watu waliouwawa wamo wanajeshi wawili wa umoja wa mataifa.Kundi la AL-SHABAB Limekiri kuhusika na tukio hilo huku wakidai kuwa Rais aliyechaguliwa,amechaguliwa na wabaya wa nchi hiyo.Hata hivyo Rais huyo mpya hakudhurika na shambulio hilo.Shambulio hilo ni shambulio la kwanza kwa kundi hilo tangu kuingia madarakani kwa Raisi huyo mpya.

Uingereza Yabanwa mbavu na Ukraine

Hatimaye goli la dakika za lala salama la Frank Lampard liliiwezesha timu ya taifa ya uingereza kupata suluhu ya 1:1 baada ya goli la mapema la Yevhen Konoplyanka katika dakika dakika ya 39...Bao hilo la lampard lilipatikana katika dakika ya 87 kwa njia ya penati baada ya mshambuliaji Danny welbeck kumshikisha mchezaji wa timu ya ukraine...

Monday, September 10, 2012

welcome

hi....am a new blogger from Tanzania...you have to look what is inside the blog..