clock

,,,,,

Friday, September 21, 2012

Makabiliano mpakani mwa Isrel na Misri

Mwanajeshi wa Israel na wapiganaji watatu wameuwawa kwenye mapigano mpakani baina ya Israil na Misri. Israel inasema wapiganaji walikuwa na silaha tele, na walifyatua risasi dhidi ya wanajeshi waliokuwa wakilinda wajenzi wanaorefusha uzio kwenye mpaka wa Israel. Inaarifiwa kuwa mpiganaji mmoja alirusha bomu.Kuna taarifa kuwa wanajeshi wengine kadhaa wa Israil walijeruhiwa. Hivi karibuni, jeshi la Misri lilifanya operesheni kubwa dhidi ya wapiganaji wa kiislamu upande wa mpaka wa Misri, baada ya shambulio Kaskazini mwa eneo la Sinai, ambapo wanajeshi 16 wa Misri waliuwawa.

No comments:

Post a Comment