clock

,,,,,

sports review

Bondia Ricky Hatton Arudi Ulingoni Ricky Hatton, bondia wa Uingereza ambaye zamani alikuwa ni bingwa wa dunia katika viwango viwili vya uzani tofauti, inaelekea huenda leseni yake ya kurudi katika ngumi ikaidhinishwa hivi karibuni. Hatton, mwenye umri wa miaka 33, alihudhuria kikao cha bodi ya ngumi, British Boxing Board of Control (BBBoC), mjini Cardiff, siku ya Jumatano, na anatazamiwa kuitisha mkutano na waandishi wa habari Ijumaa. Katibu mkuu wa bodi, Robert Smith, aliielezea BBC kwamba: "Leseni yake atarudishiwa, mara tu baada ya kukaguliwa hali yake ya afya. "Alizungumza vyema, anaonekana kuwa mwenye afya nzuri, na angelipenda kwa mara nyingine kushangiliwa." Hatton, ambaye alibandikwa jina la utani 'The Hitman', yaani 'mgongaji', hajawahi kupigana tena tangu aliposhindwa kwa KO katika raundi ya pili, alipotandikana na Manny Pacquiao mwezi Mei, mwaka 2009. Mwaka 2010, bodi hiyo ya ngumi ilimpokonya Hatton leseni, kufuatia madai ya kutumia dawa ya kulevya ya cocaine. "Anaonekana yuko katika hali nzuri kabisa, hana shida yoyote, na inaelekea hana matatizo yoyote," alielezea Smith. "Kutokana na matamshi yake, inaelekea ametulia vyema na familia yake. Tayari ameshapitia ukaguzi fulani wa kimatibabu, na tumo katika kuhakikisha anakamilisha utaratibu mzima."

3 comments:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Hatimaye leo simba wamelamba koni ..baada ya kuwatandika Azam fc kwa goli 3:2....magoli ya azam yalifungwa na john boko almaarufu kama Adebayor na kipre cheche huku simba wakiamka baadaye na kutoka nyuma ya magoli mawili ya azam na kujipatia magoli yake kupitia kwa samwel akuffor aliyefunga kwa mkwaju wa penalt,Emmanuel okwi akaipatia simba goli la kusawazisha...huku Mwinyi Kazimoto akifanya kazi ya ziada ya kuwachambua mabeki kabla ya kufumua shuti lililomwacha goli kipa wa Azam Deogratius Munishi(Dida) na kuzama wavuni...na kuiandikia Simba sports club goli la 3 ambalo ndiyo lilikuwa bao la ushindi...mpaka Mpira unaisha simba 3: 2 Azam..

    ReplyDelete
  3. Mbuyu twite na Kelvin yondani ruks yanga
    Hatimaye lile Vuguvugu la usajili lililopamba moto na kushika kasi kwa wiki kadhaa hatimaye leo,limefikia mwisho kwa kuhalalishwa kwa wachezaji mbuyu twite na kelvin yondani kuichezea timu ya yanga sports club...kwa mujibu wa habari toka kwa mwenyekiti wa tume ya haki na sheria bwana Alex mgongolwa..."kulingana na hoja na sheria Mbuyu twite na kelvin yondani ni wachezaji halali wa dar es salaam young afrika....wakati huo huo mwenyekiti wa simba sports club bwana Ismail Aden Rage amesema kuwa....Binafsi hakuridhishwa na maamuzi ya kamati hiyo...na anachofikiri ni kwa timu yake kujitoa katika kushiriki ligi kuu Tanzania bara ...maana anaona kubaki katika ligi hiyo ni mwanya kwa timu yake kuendelea kuathiriwa na maamuzi mabovu...yanayotolewa na chama chenye dhamana ya soka nchini...hivyo yuko tayari kuitisha mkutano mkuu wa wanachama na wao ndiyo wataamua aidha wabaki au wajitoe katika ligi......

    ReplyDelete