clock
,,,,,
Monday, November 26, 2012
......Nyota iliyong'aa na Kuzimika ghafla......
Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo Milionea, ""anakaririwa Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza” Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei. Kwenye gari alikua mwenyewe.""…
Yanaweza kuwa ni maneno machache lakini yamebeba ujumbe mzito ambao utasababisha wengine wapate mshtuko wa moyo na hata wengine wanaweza poteza maisha kutokana na maneno haya...Hatuna la kufanya kuzuia hayo maana kazi yake mola siku zote haina makosa.......Hussein Mkieti maarufu kama sharo milionea ilikuwa ni nyota changa iliyoanza kung'aa katika fani ya maigizo ya vichekesho na muziki wa kizazi kipya,ni watu wachache wanaoweza kumudu hivyo vyote pasi na kubase upande mmoja.Kifo chake ni kuzimika ghafla kwa nyota hiyo iliyoanza kung'aa....Tutaendelea kukukumbuka daima na milele na kukuombea kwa MWENYEZI MUNGU akulaze mahala ambapo ni salama.POLE ziende kwa familia yake,ndugu na jamaa zake na mungu awape roho za uvumilivu katika kipindi hiki kigumu walichokuwa nacho....""JEMBE LITAKUMBUKWA DAIMA""..
Uvutaji sigara 'unaozesha' ubongo
Kuvuta sigara “kunaozesha” ubongo kwa kuathiri vibaya kumbukumbu, uelewa wakati wa masomo na uwezo wa kushauriana. Hii ni kulingana na wachunguzi wa King’s College, nchini Uingereza.
Uchunguzi wa watu 8,800 wenye umri wa zaidi ya miaka 50 ulionyesha kwamba shinikizo la damu na uzito kupita kiasi pia ziliathiri ubongo, lakini kwa kiwango cha chini zaidi.
Taarifa zinazohusiana
afya
Wanasayansi walisema ni sharti watu wajue kwamba hali ya maisha inaweza kuathiri vibaya ubongo pamoja na mwili.
Wachunguzi nchini Uingereza walikuwa wanachunguza uhusiano kati ya hali ya ubongo, na visa vya shtuko wa moyo na kiharusi.
Shirikisho la kuhamasisha kuhusu ugonjwa wa Alzheimer, unaoathiri ambavyo watu wanakumbuka mambo, ulisema: "Sote tunafahamu ya kwamba uvutaji sigara, kuweko kwa shinikizo la damu, kipimo cha Cholesterol au kiwango cha juu cha mafuta mwilini, huathiri vibaya moyo. Uchunguzi huu unadhihirisha kwamba vyote hivi pia vinaathiri ubongo.
"Ni sharti watu wale chakula chenye lishe bora, wawe na uzito wa kadri, wafanye mazoezi mara kwa mara, wapimwe shinikizo la damu na cholesterol, na pia wasivute sigara."
Kuvuta sigara “kwaozesha” ubongo kwa kuathiri vibaya kumbukumbu, masomo na uwezo wa kushaurianana, kulingana na wachunguzi wa King’s College, London.
Uchunguzi wa watu 8,800 wenye umri wa zaidi ya miaka 50 ulionyesha kwamba shinikizo la damu na uzito uliopita kiasi pia ziliathiri ubongo, lakini kwa kiwango cha chini zaidi.
Wanasayansi walisema ni sharti watu wajue kwamba hali ya maisha inaweza kuathiri vibaya ubongo pamoja na mwili.
Wachunguzi wa King's College walikuwa wanachunguza uhusiano kati ya hali ya ubongo, na visa vya mshtuko wa moyo na kiharusi.
shirikikisho la kuhamasisha ugonjwa wa Alzheimer, unaoathiri kumbumkumbu, ulisema: "Sote tunafahamu ya kwamba uvutaji sigara, kuweko kwa shinikizo la damu, kipimo cha cholesterol cha juu, huathiri vibaya moyo. Uchunguzi huu unadhihirisha kwamba vyote hivi pia vinaathiri uongo.
"Ni sharti watu wale chakula chenye lishe bora, wawe na uzito wa kadri, wafanye mazoezi mara kwa mara, wapimwe shinikizo la damu na cholesterol, na pia wasivute sigara."(for more info link BBCSwahili.com)...
Thursday, November 22, 2012
Rais Kabila kushauriana na waasi wa M23
Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesema yuko tayari kuchunguza malalamishi ya wapiganaji wa waasi ambao wameuteka mji wa Goma, Mashariki mwa nchi hiyo.
Akiongea baada ya mazungumzo yaliyofanyika nchini Uganda na Kuhudhuriwa na rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais Joseph Kabila amesema anatathmini uwezekano wa kuanzisha mazungumzo na waasi hao wa M23.
Mwenyekiti na mwenyeji wa Mazungumzo hayo, rais wa Uganda Yoweri Museveni, rais Kabila na Kagame kwa kauili moja walitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano hayo na pia kutoa amri kwa waasi hao kuondoka Goma mara moja.
Awali wapiganji hao wa waasi walitishia kuendeleza mapigano hayo hadi mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa.
Hapo jana, wapiganaji hao wa M23 waliuteka mji wa Sake, ulioko takriban kilomita 27, kutoka Goma.
Ripoti zinasema wapiganaji hao sasa wanajiandaa kuelekea eneo la Kusini hadi Bukavu, takriban kilomita 230 kutoka Goma.
Kamanda mmoja wa waasi hao, aliliambia umati wa watu waliokusanyika katika uwanja wa michezo mjini Goma, kuwa safari yao ya kukomba taifa hilo imeanza.
Lakini mwandishi wa BBC mjini Goma, anasema haijabainika wazi ikiwa wapiganaji hao wa waasi wana uwezo wa kutekeleza vitisho vyao.
Kundi hilo la M23 liliundwa mwezi April mwaka huu baada ya wanajeshi kadhaa kuasi.
Wapiganaji hao wa waasi wanasema hawakupewa nyadhifa za kijeshi walizohaidiwa baada ya kusainiwa kwa mkataba wa amani mwaka wa 2009.
Vitendo vya wapiganaji hao wa M23, vimezua wasi wasi wa kuzuka upya kwa mapigano nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako takriban watu milioni tano waliauawa kufuatia mapigano yaliyoanza mwaka wa 1997 na kumalizika mwaka wa 2003.[for more info@BBCSwahili]...
Thursday, November 8, 2012
MWANAMITINDO ALBINO
Diandra Forrets akijiandaa kwa maonyesho ya mitindo nchini Afrika Kusini
Nyuma ya ukumbi, kelele zikiwa zimejaa katika tamasha la Wiki ya mitindo Afrika nchini Afrika Kusini, mwanamke mmoja amekaa kimya.
Wanamitindo wenzake pamoja na wabunifu wa mitindo kutoka kote barani Afrika wana kazi nyingi si haba. Kuna shughuli si haba kiasi cha mtu kusema kuwa kuna ushindani wa kelele.
Taarifa zinazohusiana
afya
Lakini licha ya kimya chake, Diandra Forrest mwanamitindo wa kulipwa raia wa Marekani, ndiye nyota ya chumba hiki.
“Ni muhimu kwangu kuwa hapa kwa sababu nataka kubadili ambavyo watu wanavyowatizama wasichana maalbino katika bara hili.” Alisema Diandra
Akiwa na ukosefu wa rangi katika ngozi yake au nywele zake, msichana huyo aliyekulia mjini New York, hususan katika mtaa wa Bronx ambao ni makao kwa wamarekani weusi, ni kawaida kwake kuwa na tabasamu.
Takriban mtu mmoja kwa kila watu 17,000 anazaliwa akiwa na hitifalu katika genetiki zake ambayo inaweza kumsababisha kuwa kipofu au kuwa na ulemavu wa ngozi.
Lakini anajua kuwa kuwepo kwake hapa katika maonyesho ya mitindo ya kiafrika, ina umuhimu mkubwa kuliko kuhoji dhana ya ''ni nini urembo?''
Katika baadhi ya nchi za afrika, hasa Afrika Mashariki, watu anbao ni Albino, wanaishi katika hofu ya kutekwa na kuchinjwa kwa sababu viungo vya miili yao vinaaminika kuwa na nguvu fulani.
"Ni muhimu kwangu sana kuwa hapa kwa sababu nataka kubadili dhana za watu kuhusu wasichana walio na ulemavu wa ngozi’’ aliambia BBC
"Nilidhani kuwa maisha yalikuwa magumu kwangu nilipokuwa mtoto, watoto wengine wakinikejeli saa zote. Kila nikienda nyumbani nilikuwa nalia’’ alisimulia Diandra.
'Apigwa na butwaa'
" Lakini hiyo sio hoja ikilinganishwa na kile ambacho watu kama mimi hupitia katika safu kama hii, hususan katika maeneo ya mashinani’’
Watengezaji wa mtindo, wa kimataifa wanawatumia maalbino sana siku hizi katika kuonyesha mitindo yao.
“Nilipogundua kuwa katika nchi kama Tanzania, maalbino kama mimi wanaishi na hofu ya kukatwa sehemu zao za mwili kwa sababu za kibiashara, nilipigwa na butwaa. Watu kama mimi wanaishi kwa hofu kila siku ya maisha yao. Inasikitisha sana.’’
Lakini inapokuja kwa mitindo ya kimataifa Bi Forrest anatoa mwelekeo.
Kama wengine, katika sanaa ya mitindo, msanii wa Afrika Kusini anayeishi uingereza, Jacob Kimmie alifurahi sana alipokutana na Bi forrest.
"Anaonekana tofauti sana na ana mvuto ambao sijawahi kuona kama mwanamitindo. Niliona kama lazima kuwa naye mwenye tamasha la leo.’’ Alisema Jacob.
Wakati huu katika safu za mitindo, kumtumia mwanamitindo Albino katika maonyesho yoyote , ni kitu kinachowika sana sasa. lakini natumai kuwa kutumia watu kama hawa kutaleta mabadiliko yatakayodumu’’
Refilwe Modiselle, mwanamitindo wa Afrika Kusini, na ambaye ni Albino aliyekulia mtaani Soweto,anakubaliana na kauli hii.
Kazi yake ya uwanamitindo ilianza tangu akiwa na umri wa miaka 13, na sasa yeye ndiye sura ya kampuni ya mitindo ya Legit na anasema kuwa wakati huo mtu yeyote aliyekuwa albino alibaguliwa sana.
"Nahisi kuwa kazi ambayo Diandra na mimi tunafanya ni kuleta mabadiliko ya kweli.’’ Anasema Modisile
Friday, November 2, 2012
Wanamgambo wavamia bunge la Libya
Wanamgambo waliojihami kwa bunduki, wamekalia bunge la Libya, kuelezea masikitiko yao kuhusiana na jinsi serikali mpya ya nchi hiyo ilivyoundwa.
Wanamgambo hao wanataka baadhi ya mawaziri kuondolewa, kwa sababu wanatuhumiwa kuwa na uhusiano na rais wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.
Malori kadhaa, yakiwa yamesheheni silaha za kutungulia ndege zimejipanga nje ya bunge la nchi hiyo.
Libya iliandaa uchaguzi wa amani mwezi Julai mwaka huu, na wanasiasa wa nchi hiyo waliafikiana kuhusu jinsi ya kubuni serikali mpya siku ya Jumatano.
Waziri Mkuu Ali Zidan alipataa uungwaji mkono kutoka kwa bunge la nchi hiyo kuhusiana na jinsi alivyowachagua mawaziri wake.
Waziri huyo mkuu aliwateuwa wanasiasa wasioegemea upande wowote na wenye misimamo ya kadri, katika baraza lake ili serikali yake ya mseto ikubalike na pande zote.
Lakini mazungumzo hayo yalivurugwa na maandamano mapema wiki hii na siku ya Jumatano, watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki, walivamia bunge la nchi hiyo na wamekuwa wakilidhibiti tangu wakati huo.
Habari Muhimu
Subscribe to:
Comments (Atom)




