clock

,,,,,

Monday, November 26, 2012

......Nyota iliyong'aa na Kuzimika ghafla......

Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo Milionea, ""anakaririwa Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza” Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei. Kwenye gari alikua mwenyewe.""… Yanaweza kuwa ni maneno machache lakini yamebeba ujumbe mzito ambao utasababisha wengine wapate mshtuko wa moyo na hata wengine wanaweza poteza maisha kutokana na maneno haya...Hatuna la kufanya kuzuia hayo maana kazi yake mola siku zote haina makosa...
....Hussein Mkieti maarufu kama sharo milionea ilikuwa ni nyota changa iliyoanza kung'aa katika fani ya maigizo ya vichekesho na muziki wa kizazi kipya,ni watu wachache wanaoweza kumudu hivyo vyote pasi na kubase upande mmoja.Kifo chake ni kuzimika ghafla kwa nyota hiyo iliyoanza kung'aa....Tutaendelea kukukumbuka daima na milele na kukuombea kwa MWENYEZI MUNGU akulaze mahala ambapo ni salama.POLE ziende kwa familia yake,ndugu na jamaa zake na mungu awape roho za uvumilivu katika kipindi hiki kigumu walichokuwa nacho....""JEMBE LITAKUMBUKWA DAIMA""..

No comments:

Post a Comment