clock

,,,,,

Thursday, November 8, 2012

MWANAMITINDO ALBINO

Diandra Forrets akijiandaa kwa maonyesho ya mitindo nchini Afrika Kusini Nyuma ya ukumbi, kelele zikiwa zimejaa katika tamasha la Wiki ya mitindo Afrika nchini Afrika Kusini, mwanamke mmoja amekaa kimya. Wanamitindo wenzake pamoja na wabunifu wa mitindo kutoka kote barani Afrika wana kazi nyingi si haba. Kuna shughuli si haba kiasi cha mtu kusema kuwa kuna ushindani wa kelele. Taarifa zinazohusiana afya Lakini licha ya kimya chake, Diandra Forrest mwanamitindo wa kulipwa raia wa Marekani, ndiye nyota ya chumba hiki. “Ni muhimu kwangu kuwa hapa kwa sababu nataka kubadili ambavyo watu wanavyowatizama wasichana maalbino katika bara hili.” Alisema Diandra Akiwa na ukosefu wa rangi katika ngozi yake au nywele zake, msichana huyo aliyekulia mjini New York, hususan katika mtaa wa Bronx ambao ni makao kwa wamarekani weusi, ni kawaida kwake kuwa na tabasamu. Takriban mtu mmoja kwa kila watu 17,000 anazaliwa akiwa na hitifalu katika genetiki zake ambayo inaweza kumsababisha kuwa kipofu au kuwa na ulemavu wa ngozi. Lakini anajua kuwa kuwepo kwake hapa katika maonyesho ya mitindo ya kiafrika, ina umuhimu mkubwa kuliko kuhoji dhana ya ''ni nini urembo?'' Katika baadhi ya nchi za afrika, hasa Afrika Mashariki, watu anbao ni Albino, wanaishi katika hofu ya kutekwa na kuchinjwa kwa sababu viungo vya miili yao vinaaminika kuwa na nguvu fulani. "Ni muhimu kwangu sana kuwa hapa kwa sababu nataka kubadili dhana za watu kuhusu wasichana walio na ulemavu wa ngozi’’ aliambia BBC "Nilidhani kuwa maisha yalikuwa magumu kwangu nilipokuwa mtoto, watoto wengine wakinikejeli saa zote. Kila nikienda nyumbani nilikuwa nalia’’ alisimulia Diandra. 'Apigwa na butwaa' " Lakini hiyo sio hoja ikilinganishwa na kile ambacho watu kama mimi hupitia katika safu kama hii, hususan katika maeneo ya mashinani’’ Watengezaji wa mtindo, wa kimataifa wanawatumia maalbino sana siku hizi katika kuonyesha mitindo yao. “Nilipogundua kuwa katika nchi kama Tanzania, maalbino kama mimi wanaishi na hofu ya kukatwa sehemu zao za mwili kwa sababu za kibiashara, nilipigwa na butwaa. Watu kama mimi wanaishi kwa hofu kila siku ya maisha yao. Inasikitisha sana.’’ Lakini inapokuja kwa mitindo ya kimataifa Bi Forrest anatoa mwelekeo. Kama wengine, katika sanaa ya mitindo, msanii wa Afrika Kusini anayeishi uingereza, Jacob Kimmie alifurahi sana alipokutana na Bi forrest. "Anaonekana tofauti sana na ana mvuto ambao sijawahi kuona kama mwanamitindo. Niliona kama lazima kuwa naye mwenye tamasha la leo.’’ Alisema Jacob. Wakati huu katika safu za mitindo, kumtumia mwanamitindo Albino katika maonyesho yoyote , ni kitu kinachowika sana sasa. lakini natumai kuwa kutumia watu kama hawa kutaleta mabadiliko yatakayodumu’’ Refilwe Modiselle, mwanamitindo wa Afrika Kusini, na ambaye ni Albino aliyekulia mtaani Soweto,anakubaliana na kauli hii. Kazi yake ya uwanamitindo ilianza tangu akiwa na umri wa miaka 13, na sasa yeye ndiye sura ya kampuni ya mitindo ya Legit na anasema kuwa wakati huo mtu yeyote aliyekuwa albino alibaguliwa sana. "Nahisi kuwa kazi ambayo Diandra na mimi tunafanya ni kuleta mabadiliko ya kweli.’’ Anasema Modisile

No comments:

Post a Comment