clock

,,,,,

Wednesday, May 29, 2013

KUKANUSHA KIFO CHA M 2 THE P


Kulingana na habari zilizopatikana katika mchana wa cku ya jana ni kuwa msanii ambaye alikuwa na LATE MANGWAIR ajulikanaye kwa jina la M 2 THE P ni kuwa amefariki dunia.Lakini jana mchana huohuo kulingana na taarifa zilizockika kutoka kwenye kituo kimoja cha redio cha nchini Tanzania ambacho kiliwasiliana moja kwa moja na daktari wa hospitali ya Hellen Joseph ya huko South Afrika kupitia kwa mtangazaji wao aliyekwenda South Afrika kulifatilia tukio hilo kwa umakini.Hivyo M 2 THE P hakufariki na hali yake yaelekea kuleta matumaini. WAKATI HUO HUO: Mwili wa marehemu Albert Mangwea umehamishiwa kwenye hospitali ya serikali kwa uchunguzi zaidi kabla haujakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu.Na pia daktari wa Hellen Joseph alisema ya kuwa ripoti ya kifo cha Mangwea bado haijatolewa na hivyo kutia shaka juu ya ripoti iliyoonekana kuzagaa kwa cku ya jana kwenye mitandao. AS a blogger napenda kuwapa pole ndugu wa Albert Mangwea na kuwaombea kwa mungu awape uvumilivu kwa kipindi hiki kigumu walichokuwa nacho.(for any comment,questions ,consultation...TYPE DOWN ON THE COMMENT BOX).

Tuesday, May 28, 2013

RIPOTI YA KIFO CHA MWANA(ALBERT MANGWEA) NA TETESI ZA KIFO CHA M TO THE P


(Ngwea na M to the P siku moja kabla ya kifo) The Medical report from Helen Joseph hospital,Dr Shirley Radcliffe confirming that albert Mangwair died from “alcohol toxicity” after drinking too much,Over-exhaustion and drugs overdose....The inquest heard that Albert 28, collapsed in the his friends home had been more than five-times the legal S.A drink drive limit with 416mg ... of alcohol per 100 millilitres of blood in his system....Radcliffe described the reasons for ICU admission included hypoxemia and one of his friend found “two empty vodka bottles [found] on the Car” and he had been suffering from the eating disorder Bulimia for several months before his death and endless partying session with little or no resting...sample taken from his stomach showed poly-drug cocktail and he overdosed Heroin,Cocaine 'crack' and cannabis 0.08gms was also found in his blood...and his death was caused by massive heart attack and respiratory failure followed by sudden Heart stop...and end up dead within seconds! Muda huo huo: Taarifa ninazosemekana kutoka nchini Afrika Kusini ni kwamba yule msanii aliyepelekwa hospitali pamoja na Mwana Hip Hop, Albert Mangwair aitwaye M to the P naye amefariki dunia leo. M2 the P alipelekwa katika hospitali ya St Hellen iliyopo jijini nchini humo kwa matibabu baada ya kukutwa amepoteza fahamu akiwa na Mangwair aliyefariki dunia jana. Miili ya marehemu hao bado ipo katika hospitali ya St. Hellen na mipango ya kuhamisha miili hiyo bado inaendelea hivi sasa.

JINAMIZI LA VIFO VYA MASUPASTAA


R.I.P mwana Albert Mangwea....Tutakukumbuka....

Tuesday, December 18, 2012

Rwanda inatoa amri kwa M23, yasema UN

Waziri wa ulinzi nchini Rwanda, ametuhumiwa kwa kuamuru uasi katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa ripoti ya wataalamu wa Umoja wa mataifa. Ripoti hiyo ya kisiri, iliyofichuliwa na shirika la habari la Reuters, inasema kuwa Uganda pia inaunga mkono waasi wa M23 ambao wamekuwa wakipigana na jeshi la DRC tangu mwezi Aprili. Taarifa zinazohusiana Rwanda Ripoti hii inakuja baada ya ripoti nyingine ya Umoja wa Mataifa kutolewa mwezi Juni ambayo ilituhumu Rwanda kwa kuunga mkono waasi hao Lakini Rwanda na Uganda zimekuwa zikikna madai ya kuunga mkono waasi wa M23. Duru zinasema kuwa katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, Rwanda imeunga mkono makundi ya waasi Mashariki mwa Congo, kama njia moja ya kupiga vita waasi wa kihutu waliokimbilia eneo hilo baada ya mauaji ya kimbari mwaka 1994. Baadhi wanatuhumu Rwanda kwa kutumia waasi kupigana vita vyake dhidi ya DRC , nchi ambayo ina utajiri mkubwa wa madini na eneo zima la Maziwa Makuu. Taarifa za hivi punde za wataalamu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa zinatoa maelezo zaidi kuhusu Rwanda kujihusisha na vita vya DRC. Maelfu ya watu wameachwa bila makao kufuatia mapigano Mashariki mwa DRC Wataalamu hao wanasema kuwa waasi wa M23 wanapokea amri za moja kwa moja kutoka kwa mkuu wa majeshi ya Rwanda, Generali Charles Kayonga, " ambaye naye anafuata amri za waziri wa ulinzi Generali James Kabarebe. Wataalamu hao pia wanasema kuwa Rwanda imekuwa ikitoa silaha kwa waasi hao na kuweka mikakati ya kusajili waasi zaidi ili kuliganya kundi hilo kuwa kubwa. Maelfu ya watu nchini DRC wamepoteza makao yao kufuatia vita hivyo kati ya waasi na wanajeshi wa Rwanda. Ripoti hiyo iliyoonwa na shirika la habari la Reuters inasema kuwa wanajeshi wa Rwanda na Uganda wamesaidia waasi wa M23 kupanua harakati zao katika eneo la Mashariki mwa DRC.{more at BBCSWAHILI}

Monday, December 10, 2012

Upinzani wapinga ushindi wa Rais Mahama

Chama cha upinzani nchini Ghana kimepinga matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu wa urais ambayo yalimpa ushindi rais John Mahama. Tume ya uchaguzi ilisema kuwa bwana Mahama alishinda kwa asilimia hamsini na saba ya kura na kuondoa uwezekano wa kufanyika duru ya pili ya uchaguzi huo dhidi ya mpinzani wake Nana Akufo-Addo aliyepata asilimia 47 ya kura. Taarifa zinazohusiana Siasa Chama cha upinzani New Patriotic Party, kimedai kutokea wizi wa kura na kusema kitafanya mkutano hapo keshi kuamua hatua watakazochukua. Ghana imejipa sifa ya kuwa nchi yenye demokrasia thabiti barani Afrika na moja ya nchi zinazokuwa kwa kasi kubwa barani Afrika. Kwa upande wake rais Mahama aliwataka watu kuheshimiana kufuatia matangazo ya kura ambayo yalimpa ushindi. Hapakuwa na ripoti zozote za ghasia Jumatatu asubuhi baada ya matangazo ya uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali kutangazwa siku ya Jumapili. Furaha na nderemo zilijaa punde baada ya matangazo, huku mamia ya watu wakijitokeza kuonyesha furaha yao kwa ushindi wa rais Mahama.

Monday, December 3, 2012

Soma Ucheke

Elimu peke yake haitoshi kumpa mtu kazi. Wanuswa kwapa kama mahojiano Hata ujuzi pia hauna maana. Huko ni China. Shirika maarufu la Uchina, HAINAN AIRLINE limeweka masharti kwamba mbali na elimu na uzoefu lazima usinuke. Ukiwa mwili wako una harufu mbaya basi kazi huna. Ni China huko. Kwa mujibu wa gazeti la SZ News shirika hilo katika kuajiri marubaNi wapya lazima mtu ananuswa makwapa. Ukiwa unakikwapa, au makwapa yako yana harufu unanyimwa kazi. Kabla ya kuajiriwa katika shirika hilo la ndege. Hatua ya kwanza ni kunuswa kwapa zako. Wakuu wa shirika hilo wanajitetea wakisema, kwa vile marubani wanafanya kazi karibu zaidi na watu basi ni lazima wasiwe na harufu ya kutisha kwani harufu mbaya ya miili yao au makwapa huenda ikawapunguzia wateja.

Monday, November 26, 2012

......Nyota iliyong'aa na Kuzimika ghafla......

Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo Milionea, ""anakaririwa Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza” Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei. Kwenye gari alikua mwenyewe.""… Yanaweza kuwa ni maneno machache lakini yamebeba ujumbe mzito ambao utasababisha wengine wapate mshtuko wa moyo na hata wengine wanaweza poteza maisha kutokana na maneno haya...Hatuna la kufanya kuzuia hayo maana kazi yake mola siku zote haina makosa...
....Hussein Mkieti maarufu kama sharo milionea ilikuwa ni nyota changa iliyoanza kung'aa katika fani ya maigizo ya vichekesho na muziki wa kizazi kipya,ni watu wachache wanaoweza kumudu hivyo vyote pasi na kubase upande mmoja.Kifo chake ni kuzimika ghafla kwa nyota hiyo iliyoanza kung'aa....Tutaendelea kukukumbuka daima na milele na kukuombea kwa MWENYEZI MUNGU akulaze mahala ambapo ni salama.POLE ziende kwa familia yake,ndugu na jamaa zake na mungu awape roho za uvumilivu katika kipindi hiki kigumu walichokuwa nacho....""JEMBE LITAKUMBUKWA DAIMA""..

Uvutaji sigara 'unaozesha' ubongo

Kuvuta sigara “kunaozesha” ubongo kwa kuathiri vibaya kumbukumbu, uelewa wakati wa masomo na uwezo wa kushauriana. Hii ni kulingana na wachunguzi wa King’s College, nchini Uingereza. Uchunguzi wa watu 8,800 wenye umri wa zaidi ya miaka 50 ulionyesha kwamba shinikizo la damu na uzito kupita kiasi pia ziliathiri ubongo, lakini kwa kiwango cha chini zaidi. Taarifa zinazohusiana afya Wanasayansi walisema ni sharti watu wajue kwamba hali ya maisha inaweza kuathiri vibaya ubongo pamoja na mwili. Wachunguzi nchini Uingereza walikuwa wanachunguza uhusiano kati ya hali ya ubongo, na visa vya shtuko wa moyo na kiharusi. Shirikisho la kuhamasisha kuhusu ugonjwa wa Alzheimer, unaoathiri ambavyo watu wanakumbuka mambo, ulisema: "Sote tunafahamu ya kwamba uvutaji sigara, kuweko kwa shinikizo la damu, kipimo cha Cholesterol au kiwango cha juu cha mafuta mwilini, huathiri vibaya moyo. Uchunguzi huu unadhihirisha kwamba vyote hivi pia vinaathiri ubongo. "Ni sharti watu wale chakula chenye lishe bora, wawe na uzito wa kadri, wafanye mazoezi mara kwa mara, wapimwe shinikizo la damu na cholesterol, na pia wasivute sigara." Kuvuta sigara “kwaozesha” ubongo kwa kuathiri vibaya kumbukumbu, masomo na uwezo wa kushaurianana, kulingana na wachunguzi wa King’s College, London. Uchunguzi wa watu 8,800 wenye umri wa zaidi ya miaka 50 ulionyesha kwamba shinikizo la damu na uzito uliopita kiasi pia ziliathiri ubongo, lakini kwa kiwango cha chini zaidi. Wanasayansi walisema ni sharti watu wajue kwamba hali ya maisha inaweza kuathiri vibaya ubongo pamoja na mwili. Wachunguzi wa King's College walikuwa wanachunguza uhusiano kati ya hali ya ubongo, na visa vya mshtuko wa moyo na kiharusi. shirikikisho la kuhamasisha ugonjwa wa Alzheimer, unaoathiri kumbumkumbu, ulisema: "Sote tunafahamu ya kwamba uvutaji sigara, kuweko kwa shinikizo la damu, kipimo cha cholesterol cha juu, huathiri vibaya moyo. Uchunguzi huu unadhihirisha kwamba vyote hivi pia vinaathiri uongo. "Ni sharti watu wale chakula chenye lishe bora, wawe na uzito wa kadri, wafanye mazoezi mara kwa mara, wapimwe shinikizo la damu na cholesterol, na pia wasivute sigara."(for more info link BBCSwahili.com)...

Thursday, November 22, 2012

Rais Kabila kushauriana na waasi wa M23

Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesema yuko tayari kuchunguza malalamishi ya wapiganaji wa waasi ambao wameuteka mji wa Goma, Mashariki mwa nchi hiyo. Akiongea baada ya mazungumzo yaliyofanyika nchini Uganda na Kuhudhuriwa na rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais Joseph Kabila amesema anatathmini uwezekano wa kuanzisha mazungumzo na waasi hao wa M23. Mwenyekiti na mwenyeji wa Mazungumzo hayo, rais wa Uganda Yoweri Museveni, rais Kabila na Kagame kwa kauili moja walitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano hayo na pia kutoa amri kwa waasi hao kuondoka Goma mara moja. Awali wapiganji hao wa waasi walitishia kuendeleza mapigano hayo hadi mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa. Hapo jana, wapiganaji hao wa M23 waliuteka mji wa Sake, ulioko takriban kilomita 27, kutoka Goma. Ripoti zinasema wapiganaji hao sasa wanajiandaa kuelekea eneo la Kusini hadi Bukavu, takriban kilomita 230 kutoka Goma. Kamanda mmoja wa waasi hao, aliliambia umati wa watu waliokusanyika katika uwanja wa michezo mjini Goma, kuwa safari yao ya kukomba taifa hilo imeanza. Lakini mwandishi wa BBC mjini Goma, anasema haijabainika wazi ikiwa wapiganaji hao wa waasi wana uwezo wa kutekeleza vitisho vyao. Kundi hilo la M23 liliundwa mwezi April mwaka huu baada ya wanajeshi kadhaa kuasi. Wapiganaji hao wa waasi wanasema hawakupewa nyadhifa za kijeshi walizohaidiwa baada ya kusainiwa kwa mkataba wa amani mwaka wa 2009. Vitendo vya wapiganaji hao wa M23, vimezua wasi wasi wa kuzuka upya kwa mapigano nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako takriban watu milioni tano waliauawa kufuatia mapigano yaliyoanza mwaka wa 1997 na kumalizika mwaka wa 2003.[for more info@BBCSwahili]...